![]() | |||
Home | www.lamecklister.org | Form |
MAHUBIRI YA INJILI KWA WATU WA KIMATAIFA
Bwana Yesu asiwe,Jina lake litukuzwe,Karibu kusoma na kutafakari mahubiri ya injili kwa watu wa kimataifa kama wafanyabiashara wa kimataifa(mashule,computer software,hoteli,kampuni za ndege,vyuo),waandishi wa habari za kimataifa,wanamichezo wa kimataifa(tenisi,mpira na riadha) kisha kuamua kuokoka.
Imeandikwa ktk matendo 8:5 -8 " Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo.Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya.Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa.Ikawa furaha kubwa katika mji ule."
Sikilizeni watu wa kimataifa,Yesu ndiye kristo,ndiye masihi aliyetabiriwa na manabii wa agano la kale kama Nabii Isaya kuwa angezaliwa na mwanamke bikira na kufa kwa ajili ya dhambi za watu zipate kuondolewa kwa damu yake na za kwako mtu wa kimataifa zikiwemo. Angejaa nguvu za mungu za kutatua matatizo yaliyoshindikana kwa watu kama uziwi.
Yesu ndiye kristo ee mtu wa kimataifa,yote yaliyotabiriwa kuhusu yeye yalitimia miaka 2000 iliyopita na yamendikwa ktk vitabu vya injili ktk biblia kama mathayo,marko na Yohana.
Yesu ndiye kristo ee mtu wa kimataifa,alijaa roho mtakatifu pasipo ukomo yaani nguvu za mungu ambazo ni majibu ya matatizo ya watu yaliyokuwa hayawekani kwa wanadamu kama kupooza,ukiwete na mapepo wachafu.
Yesu ndiye kristo ee mtu wa kimataifa,ndiye mfalme anayetawala wanadamu wamwaminio mungu wa kweli ktk ulimwengu wa roho kwa njia ya yeye.
Yesu ndiye kristo ee mtu wa kimataifa,alijaa roho mtakatifu yaani roho ya mungu aliyemuongoza siku zote za maisha yake asitende dhambi na Yesu alitii maongozi yake hivyo hukufanya dhambi ktk maisha yake.Naye humpa kila atubuye kwa jina lake na kumwani roho mtakatifu.
Ee mtu wa kimataifa, je waamini Yesu wa Nazareth ndiye kristo? U tayari kutubu dhambi kwa jina lake na kumtii roho mtakakatifu atakayekupa? Kama ndiyo fuatisha sala hii kwa imani;
"Bwana Yesu mimi ni mwenye dhambi,natubu dhambi za tangu kuzaliwa,nisamehe na uniondolee kwa damu yako nipe roho wako mtakatifu.Yesu ingia ndani ya nafsi yangu na uandike jina langu mbinguni.Ameni"
Sasa umeokoka ee mtu wa kimataifa,Yesu amekuwa kristo kwako una haki ya kuomba tatizo lako liloshindikana kwa wanadamu naye akatenda maana umekuwa mwana mbele za mungu.Nakushauri tafuta kanisa/huduma ya kanisa ya wakristu waliokoka kama zile za mitume,manabii,waalimu,wachungaji na wainjilisti uende na kumwabudu/kumtumikia Bwana Yesu na Mungu ambaye Baba yake. Pia tafuta mafundisho ya kukua kiroho(wokovu) ili upate kumfahamu sana Yesu na kumjua sana mungu upate kuwa mtumishi wake.
Neno la mungu Yesu wangu abariki na kukutajirisha wewe uliyeokoka ajaze maisha yako mema yake.Ameni.
Holy spirit foundation teaching | Testimonies of saved christians | Advertisement |
Contact Us; email : listlameck5@gmail.com mob: +255658601034 or +255695672865 P.Box 9332 |